Genesis 36:1-6

Wazao Wa Esau

(1 Nyakati 1:34-42)

1Hivi ndivyo vizazi vya Esau (yaani Edomu).

2Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti wa Eloni Mhiti, Oholibama binti wa Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi, 3pia akaoa Basemathi binti wa Ishmaeli, dada yake Nebayothi.

4Ada akamzalia Esau Elifazi, Basemathi akamzaa Reueli, 5Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani.

6Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike na wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake.
Copyright information for SwhKC